Simba SC imeibonda Mashujaa FC kipigo cha mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam.
Wa kwanza kufunga ni Libasse Gueye, akafuata Elie Mpanzu aliyefunga mawili.. huku wengine wakiwa ni Anicet Oura, Morice Abraham na Ismael Olivier Toure…
Goli la kufutia machozi ni la maajabu kutoka kwa Selemani Bwenzi…
Tazama magoli yote saba, na kadi nyekundu waliyopata Mashujaa FC kupitia kwa straika wake Hassan Kabunda.